2014-02-02 10:23:09

Shirika la Masista Bibi Yetu Malkia wa Afrika


Mama Kanisa anapoadhimisha Siku kuu ya kutolewa Bwana Hekanuni, Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inapenda leo kukushirikisha historia fupi ya Shirika la Masista Bibi yetu Malkia wa Afrika, kutoka Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Tanzania. Tutaangalia pia karama ya Shirika, kauli mbiu, utume na changamoto wanazokabiliana nazo kwa ufupi. RealAudioMP3

Basi akawaambia “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari njema kwa watu wote. Anayeamini na hubatizwa ataokolewa. Asiyeamini atahukumiwa.” (Mark.16:15-16). Shirika letu ni Shirika la kitawamrengo kijimbo, katika Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Tanzania, lijulikanalo kama Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika, ambamo washirika wake wanajiweka wakfu kwa Mungu.

Watawa wanafuata mausia kiinjili kwa kujifunga wenyewe na Nadhiri hadhara za Usafi moyo kamili, Ufukara na Utii. Shirika lilianzishwa mwaka 1903 na Mhasham Askofu Adolf Lechaptois, mwanachama wa Wamisionari wa Afrika (White Fathers ), Mama mlezi wa kwanza akiwa Sr. Philipa (White Sisters). shirika ilisajiliwa Roma mwaka 1949 chini ya uongozi wa Mhashamu Askofu James H. Sidle. Wanashirika wanaishi katika nyumba za kitawa wakitawaliwa na kuongozwa na roho ya mwanzilishi, Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, Sheria za Kanisa pamoja na miongozo na taratibu zilizoainishwa na Katiba ya shirika.

Karama ya Masista wa Mama yetu Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika ni uinjilishaji, yaani kufundisha na kuhubiri Habari za Ufalme wa Mungu Ufalme wa amani, haki na mapendo. Kwa kufanya hivyo shirika linafuata nyayo za Kristo Mwalimu pekee na wakati huohuo kuitikia mwito na mwaliko wake.”Basi nendeni ulimwenguni mkayafanye mata yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” (Mat.28:19). Wanashirika ni mawakala na wahamasishsji wa tunu za falme wa Mungu, tunu za haki, amani na upendo.

Masista wa shirika hili wanajitoa kumtumikia Mungu na watu wote kwa unyenyekevu wakifuata mfano wa Mama Bikira Maria msimamizi, mlinzi na mlezi wao. Kwa hiyo, kiini kabisa cha shirika letu ni kuhubiri Ufalme wa Mungu na kuufanya ujulikane kwa watu. Ufalme wa Mungu ni Ufalme wa mapendo, na kwa jinsi hiyo wanashirika popote walipo wanaalikwa kumpenda MUNGU na KUWAPENDA JIRANI ZAO. Wanashirika wanayatekeleza hayo kwa njia ya elimu ya Dini yaani Katekesi, ualimu (elimu ya dunia), uuguzi, kutunza yatima na weye shida, wakiongozwa na roho ya mwanzilishi, roho ya kuwasaidia watu kumjua na kumpenda Kristo na jirani.

Kauli mbiu yao ni upendo kwa wote. Wanashirika hujitoa wenyewe kumtumikia Mungu na watu kwa njia ya: Nadhiri Utii, Ufukara na Usafi moyo kamili. Shirika linajitahidi kumfanya Mungu na Ufalme wake ujulikane kwa watu wote kwa njia ya utume mbalimbali:

• Kutangaza Habari Njema kwa watu wote kwa njia ya katekesi na kwa njia ya maisha ya kitutume.

• Kufundisha dini mashuleni na kuwaanda wanakanisa wanaojiandaa kupokea sakramenti mbalimbali za kanisa maparokiani (ubatizo, Comunio ya kwanza Kipaimara na Ndoa),na kufund elimu ya kawaida mashuleni na katika mazingira yasiyo ya darasani.

• Kutoa huduma za afya kwa wagonjwa katika dispensari, vituo vya afya na mahospitalini na kufundisha elimu ya afya kwa jamii hasa akina mama na vijana mashuleni na pia kutoa ushauri nasaha kwa wenye VVU / UKIMWI na walioathirika kisaikolojia.

• Kutunza yatima, watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, fukara na walemavu na wazee. Kufundsha elimu ya kujitegemea na ubunifu kwa njia ya Home craft (elimu ya maarifa ya nyumbani kwa vitendo) katika vikundi vya akina mama na vijana. Kupeleka huduma kwa watu kwa kuangalia mahitajika yao ya msingi.

Changamoto.
Miito: wasichana wanao itikia wito huu mtakafu idadi kubwa ni wale waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne, wale wa kidato cha nne wakati mwingine ni wale ambao hawakufaulu viziri. Kwa hiyo shirika linakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwaendeleza masista kielimu. ka tunavyojua gharama ya kusomesha ilivyo kubwa.

Malezi:
Shirika lina walezi wazuri wenye sifa na waliopitia kozi mbalimbali za kulea miito ya utawa. lakini ubora wa miito hautegemei walezi peke yao bali malezi ya nyumbani ni muhimu sana kabla ya kuingia utawa.Wadau wote wa kukuza miito mitakatifu maparokiani: Mapadre, masista makatekista wzazi na jumuiya ndogondogo za Kikkristo tunapaswa kushirikiana wote kulea na kuelekeza vijana kuishi maisha safi ya kikristo tangu wakiwa wadogo.

Kiuchumi:
Shirika letu bado ni la kijimbo, hivyo kujiendesha kwake kunategemea wanashirika wenyewe tu. katika umaskini na unyonge huo bado shirika linakabiliwa na mzigo mzito wa kuwatunza wanashirika wagonjwa na wazee, pamoja na watoto yatima. Ili kijikimu, mbinu za uanzishaji katika miradi midogomodogo na hata mikubwa zinahitajika, pamoja na kuwa na kianzio cha kutosha.

Hata hivyo tunawashukuru baadhi ya watu wenye mapenzi mema na utume huu wa Kristo wanaotusaidia walau katika kuwatunza yatima na katika jitihada zetu za kupeleka huduma za jamii kwa watu. Bado tunawahitaji wenye moyo kama huo. Na Mungu awabariki sana.
Wanashirika kwa sasa wanafanya utume wao nchini Tanzania na Zambia. Kwa Tanzania Shirika la Masista Bibi Yetu Malkia wa Afrika wako: Sumbawanga, Mpanda, Kigoma, Jimbo kuu la Tabora, Jimbo kuu la Mwanza, Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mbeya na Moshi.








All the contents on this site are copyrighted ©.