2014-01-30 11:33:51

Si habari kumsifia Papa Francisko na kumtupia "madongo" Benedikto XVI!


Padre Federico Lombardi msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuwa na mvuto mkubwa kwa vyombo mbali mbali vya upashanaji habari. Wengi wanachambua mambo mazuri yanayofanywa na Baba Mtakatifu Francisko katika kulinda na kuwatetea wanyonge na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.

Hili ni jambo jema kama ambavyo Jarida la "Rolling Stone" lilivyoandika na habari zake kusambaa kama umande wa asubuhi. Padre Lombardi anasema, inasikitisha kuona kwamba, Jarida hili linaandika mambo mazuri ya Papa Francisko wakati huo huo linamtupia "madongo" Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI.

Huu si uandishi wa habari wenye tija wala mashiko kwa Papa Francisko anayetambua na kuthamini mchango mkubwa uliofanywa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI katika maisha na utume wa Kanisa!







All the contents on this site are copyrighted ©.