2014-01-30 10:19:54

Mshikamano wa Papa Francisko na wahanga wa ajali ya moto nchini Canada!


Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni alituma salam za rambi rambi kwa Askofu mkuu Pierre-Andrè Fournier wa Jimbo kuu la Rimouski, Canada kutokana na ajali ya moto uliounguza makazi ya wazee huko Lisle Verte na hivyo kusababisha watu 32 kupoteza maisha, wengine wengi kujeruhiwa na wengi hadi sasa hawajulikani waliko.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu umeandikwa kwa niaba yake na Kardinali mteule Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican na kwamba, Baba Mtakatifu yuko karibu na wote waliofikwa na msiba huu kwa njia ya sala. Anapenda kuwazamisha wote waliofariki dunia katika huruma ya Mungu ili waweze kuina nuru ya uzima wa milele. Baba Mtakatifu anapenda kuzifariji familia na wote waliopata majeraha na kwamba, anawaombea ili waweze kupona haraka.

Baba Mtakatifu anakipongeza kikosi cha zimamoto kwa kazi kubwa kilichofanya katika jitihada za kuokoa maisha ya watu na mali zao. Wote hawa anawapatia baraka zake za kitume!







All the contents on this site are copyrighted ©.