2014-01-28 14:30:02

Ubatizo na Msalaba vinawaunganisha Wakristo!


Wakristo wanaendelea kuhamasishwa kusali kwa ajili ya umoja wa Wakristo kwani utengano bado ni kashfa kubwa inayozuia ushuhuda wa pamoja miongoni mwa Wakristo katika mchakato wa utangazaji wa Habari Njema ya Wokovu.

Hivi karibuni, Wakristo wamefunga juma la kuombea Umoja wa Wakristo, tafakari kwa Mwaka huu iliandaliwa na Wakristo kutoka Canada kwa kuongozwa na kauli mbiu "Je, Kristo amegawanyika!"

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawaalika waamini kusali kwa ajili ya kuombea Umoja wa Wakristo. Kuna mambo msingi yanayowaunganisha Wakristo! Ubatizo na Msalaba wa Kristo!







All the contents on this site are copyrighted ©.