2014-01-28 09:08:32

Papa kuadhimisha Siku ya Watawa Duniani, Jumapili 2 Februari 2014 mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni sanjari na Siku ya Watawa Duniani, Jumapili ijayo tarehe 2 Februari 2014, kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Tiketi za kuingilia kwenye Ibada hii zinapatikana kwenye Ofisi za Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume iliyoko mjini Roma kuanzia Alhamisi tarehe 30 hadi Ijumaa tarehe 31 Januari 2014, kuanzia saa 2:30 hadi saa 7: 00 Mchana.







All the contents on this site are copyrighted ©.