2014-01-25 11:44:33

Jifunzeni kushukuru!


Kwa kawaida binadamu ni mwepesi mno kupiga magoti kumlilia na kumwomba Mwenyezi Mungu katika shida na mahangaiko yake ya ndani. Hili ni jambo linalofanywa na wengi. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema, Je, waamini watajifunza lini kurudi na kumshukuru na kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa ukarimu na wema anaoendelea kuwatendea waja wake?

Wataalam wanasema, Falsafa ya Neno asante ni kuomba tena! Waamini wajifunze kuomba, kushukuru na kumwabudu Mungu katika roho na ukweli! Tarehe 25 Januari, Kanisa linaadhimisha Siku kuu ya Wongofu wa Mtume Paulo, mwalimu wa Mataifa. Ni kipindi cha kumshukuru na kumwabudu Mungu kwa wema na ukarimu wake katika mafanikio yaliyokwishakupatikana katika mchakato wa majadiliano ya Kiekumene miongoni mwa wafuasi wa Kristo!







All the contents on this site are copyrighted ©.