Jengeni madaraja ya mazungumzo, sio kuta za chuki na fitina
Wakristo ni lazima kujenga madaraja ya mazungumzo, na sio kuta za chuki na fitina.
Baba Mtakatifu Francisko alihimiza wakati wa Ibada ya Misa ya asubuhi ya Ijumaa aliyoongoza
katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, mjini Vatican. .
Papa Francisko alitafakari
somo la Somo la kwanza juu ya mgogoro uliokuwepo kati ya Mfalme Sauli na Daudi, akisema
kuna wakati Daudi alipata na nafasi ya kumuua Sauli, lakini, hakufanya hivyo, badala
yake alichukua maamuzi ya kufuata njia ya mazungumzo, kufanya amani.
Na ndivyo
inavyotakiwa kwa Wakristo wote duniani, lazima kufuata njia ya majadiliano na maafikiano
kwa amani, kwa sababu Yesu alitufundisha kufanya hivyo. Wapendeni adui zenu na waoombeeni.
Yeye mwenyewe Yesu akiwa msalabani aliwaombea adui zake akisema, Baba Wasamehe maana
hawajui walifanyalo. Hivyo ndivyo Yesu anavyotaka tuwasamehe na kuwaombea wale wanao
tuchukia. Yesu ametuonyesha njia hii, kwmaba ni kuingia katika majadiliano katika
hali ya upole na unyenyekevu, licha ya mashambulizi makali. Ni muhimu , kuwa mnyenyekevu
na mlaini lakini bila kukubali kupokonywa imani kwa Yesu, Bwana wa Upatanisho.
Papa
alieleza huku akionyesha kutambua kwamba, ni kweli siyo rahisi kujenga hali ya mazungumzo,
hasa wakati wa migawanyiko mikali ya chuki.Sote tunafahamu kuwa upole na unyenyekevu
, hukimeza kiburi cha mwingine, na ni muhimu kufanya hivyo, kwa sababu, kwa njia
hiyo, polepole amani na kuheshimiana huanza kujengeka .
Kujinyenyekeza pengine
huwa ni vigumu , lakini Mkristu anapaswa kutambua kwamba, kuruhusu chuki kuvimba
moyoni ni mbaya zaidi kuliko kuanza kujenga madaraja ya majadiliano. Kuruhusu chuki
kukua, huongoza katika hali ya upweke na uchungu mkali wa uadui wenyewe. Kuwa Mkristo,
hivyo maana yake ni kuwa mjenzi wa madaraja ya mazungumzano. Ni muhimu , Papa
Francisko aliendelea , kutoruhusu muda mrefu kupita baada ya dhoruba za chuki na
kushambuliana kutokea. Ni vyema kujenga mazungumzo haraka iwezekanavyo , kwa ajili
ya kuzuia kuta za chuki kukua ni kama vile mkulima asivyoruhusu magugu kukua katika
shamba lake la nafaka. Ukuta wa chuki ukisha kuwa mkubwa , inakuwa ni kazi ngumu
kuubomoa na kujenga maridhiano. Papa alihitimisha kwa kuonyesha hofu yake katika
uwepo kuta zinazojengeka kila siku, kuta za chuki na fitina za muda mrefu, akiomba
Wakristu wote wafuate mfano wa Daudi , ambaye alishinda chuki kwa kitendo cha unyenyekevu.
.