Misri haikualikwa Ikulu ya Marekani wakati mkutano wa wakuu wa Nchi za Kiafrika mwezi
Agosti, 2014
Serikali ya Misri imesikitishwa na kitendo cha Ikulu ya Marekani kutoialika kushiriki
katika mkutano kati ya Serikali ya Marekani na Viongozi wakuu wa Serikali kutoka Barani
Afrika, utakaofanyika mjini Washington DC, kati ya tehe 5 na 6 Agosti 2014. Waziri
wa mambo ya nchi za nje wa Misri anasema, uamuzi huu si wa busara na wala hauna mtazamo
mpana.
Ikulu ya Marekani imejibu shutuma hizi kwa kusema kwamba, uamuzi huu
hauna sababu zozote za kisiasa.
Itakumbukwa kwamba, Misri ilisimamishwa kuwa
mwanachama wa Umoja wa Afrika baada ya kumwondoa kutoka madarakani Rais Mohammed Mursi
aliyekuwa amechaguliwa kidemokrasia.