2014-01-23 10:35:23

Viongozi wa Nchi za Kiafrika kukutana na Rais Obama mjini Washington DC, Agosti, 2014


Rais Barack Obama wa Marekani ametuma mwaliko kwa wakuu wa Nchi za Kiafrika kushiriki katika mkutano maalum utakaofanyika Washington DC, kati ya tarehe 5 hadi tarehe 6 Agosti 2014. Ikulu ya Serikali ya Marekani inasema kwamba, lengo la mkutano huu ni kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na Bara la Afrika linaloendelea kukua na kucharuka kwa maendeleo ya kiuchumi.

Katika mkutano huu, Marekani itafafanua maendeleo yaliyokwishafikiwa tangu Rais Barack Obama wa Marekani alipofanya mara ya mwisho ziara ya kikazi Barani Afrika. Mkazo ni katika ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji Barani Afrika. Marekani itaendelea kuunga mkono juhudi za Bara la Afrika katika masuala ya ulinzi na usalama.







All the contents on this site are copyrighted ©.