2014-01-23 15:28:51

IOR inaendelea kutenda kwa uwazi zaidi- Vatican


Siku ya Jumatano, Taasisi inayosimamia masuala ya kifedha katika Mashirika Katoliki (IOR ) - inayojulikana kama "Vatican Bank" – ilitoa tamko lake kwa vyombo vya habari juu ya hatua zilizopigwa kuelekea utendaji ulio wazi zaidi na miongozo ya kufuatwa. Tamko hilo kimsingi lilitoa maelezo ya kiufundi juu ya hatua zilizochukuliwa na juu ya mageuzi kwa siku zijazo.
Rais IOR, Ernst von Freyberg, akijibu katika mahojiano na Stefan von Kempis wa Radio Vatican, ni nini kilicho kipya katika uwazi na kanuni za utendaji wa IOR , alirejea tamko la IOR la Mei 2013, ambamo waliitangazia dunia kwamba, watajaribu kuondoa lawama zote na kuwa wazi zaidi. Amesema kwa wengi ilionekana kama ni jambo lisilowezekana. Lakini mageuzi hayo yamewezekana, na yametoa nafasi kwa Papa kuchagua hali ya baadaye IOR .
Na kwamba, wametumia uzoefu wa kipindi cha nyuma kutengeneza mfumo mpya na kuchambua utendaji wa wateja wao, kw aajili ya kurekebisha makosa kwa kadri inavyowezekana. Na ameutaja mfumo huo kuwa ni kati ya IOR na mamlaka Vatican, na kutoka kwa mamlaka Vatican hadi ushirikiano wa kimataifa na mamlaka nyingine zinazohusika kaika juhudi hizi za kuzuia utakatifushaji wa fedha katika mipango michafu .
Na kwamba kwa upande wa IOR, ni kuwa na taratibu na vitabu vya miongozo vitakavyowezesha kutambua shughuli mbovu wakati wa uhamishaji wa fedha , na pia kuwa na mfumo sahihi , na kutoa mafunzo kwa watu wanao fanyakazi katika mfumo huu.
Hatua inayofuatia katika mfumo huo ni kutoa matokeo ya utafiti wao kwa mamlaka husika. Na mpaka sasa wamepiga hatua kubwa katika uboreshaji wa mchakato huu, na katika Taarifa za IOR. Na tokea hapo , wanaingia katika hatua nyingine ya ushirikiano wa kimataifa, kama ilivyoonekana katika kesi Scarano. Lakini akasema, si kazi yake kutangaza hadharani, matokeo ya utafiti wao katika kesi binafisi.
Na kwamba kwa mwaka 2014, wana mengi ya kufanya juu ya uwazi na utaratibu wa kufuata, ingawa tayari wamepiga hatua mbele zaidi za kimaendeleo kuliko hata walivyofikiri. Na kwa wakati huu wanasubiri maamuzi na ufafanuzi zaidi kutoka kwa Baba Mtakatifu juu ya hali ya baadaye ya IOR .








All the contents on this site are copyrighted ©.