2014-01-22 07:13:48

Siku ya Vijana Kitaifa Rwanda


Vijana Wakatoliki nchini Rwanda, Jumapili tarehe 26 Januari 2014 wanaadhimisha Siku ya tisa ya Vijana Kitaifa, inayoongozwa na kauli mbiu “Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa Mungu ni wao.” RealAudioMP3

Hii ndiyo mada iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kunako Novemba 2013 kama changamoto ya mwendelezo wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani iliyofanyika mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kitaifa nchini Rwanda kwa mwaka huu yana maana ya pekee kwani Tume ya shughuli za kichungaji kwa vijana kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Rwanda, inasherehekea Jubilee ya Miaka 25 tangu ilipoanzishwa, kunako tarehe 21 Septemba 1989.

Kilele cha Jubilee hii kinatarajiwa kufanyika Mwezi Septemba, 2014 mjini Kabgayi, baadaye, Mwezi Novemba, Jimboni Byumba, kutafanyika Jukwaa la Vijana Rwanda, Jukwaa ambalo linatarajiwa kuhudhuriwa na vijana kutoka Madhehebu mbali mbali ya Kikristo kutoka ndani na nje ya Rwanda.








All the contents on this site are copyrighted ©.