2014-01-22 15:05:06

Maadhimisho ya Siku Kuu ya Mtakatifu Anyesi- Papa apokea wana kondoo


Jumanne , ambayo ilikuwa ni Siku Kuu ya Mtakatifu Agnes, Papa Francisko alipokea wanakondoo ambao manyoya yao yatatumika kutengeneza kitambaa cheupe cha kuvaa shingoni kinachotumiwa na Papa na Maaskofu wakuu, maarufu kwa jina la Pallium.
Uwasilishaji wa wana kondoo hao ilikuwa ni sehemu ya utamaduni unaofanyika kila mwaka katika maadhimisho ya Liturujia ya Siku Kuu ya Mtakatifu Angnes . Wanakondoo hao hufungwa na Masista wa Mtakatifu Lorenzo wa Panisperna wanaoishi katika eneo la kanisa la mjini Roma, alikozikwa Mtakatifu Agnes.

Manyonya ya wanakondoo hao , hufumwa katika mtindo wa kitambaa cheupe chembamba “Palium” ambacho hupambwa na misalaba sita myeusi , na huvaliwa katika Ibada za Kiliturujia na Papa na Maaskofu Wakuu, katika Makanisa yao. Pallium hizo, huhifadhiwa karibu na madhabahu ya kitubio ya Mtakatifu Petro, na hutolewa na Papa kwa Maaskofu Wakuu wapya katika Ibada ya Maadhimisho ya siku Kuu ya ni Watakatifu Petro na Paulo, kama ishara ya muungano na Kiti cha Kitume.

Watawa katika Nyumba ya Mtakatifu Lorenzo wa Panisperna , walipewa upendeleo huo wa kufunga kondoo na kuwatoa kwa Papa kwa mujibu wa Sheria ya Kanisa, ya maadhimisho ya sikukuu ya Mtakatifu Agnes, shahidi mfia dini wa mwaka 305, ambaye huchukuliwa kama ishara ya mwana-kondoo.










All the contents on this site are copyrighted ©.