2014-01-21 15:27:51

Papa ahimiza kutunza unyenyekevu katika mazungumzo na Bwana.


Baba Mtakatifu Francisko amehimiza waamini kutunza soni na unyenyekevu, wakati wa mazungumzo na Bwana, kwa kuwa Bwana hujenga mahusiano na watu wanyenyekevu na wapole wasiotaka makuu wala kujitukuza. Na daima ni mahusiano binafsi , mahusiano ya ndani ya mtu mwenyewe na Mungu.

Papa alitoa msisitizo huo, mapema asubuhi Jumanne hii wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Na hasa alizungumzia mahusiano ya mtu binafsi na Mungu na watu wake. Alisema, Bwana daima huwa na uhusiano binafsi na kila mmojawetu. Bwana , hasa hutafuta kujenga mahusiano na watu wapole na wanyenyekevu wasiotaka kujikuza, lakini wale watu maskini wasiokuwa na uwezo au mamlaka katika jamii, wale walio tupwa pembezoni na jamii , wenye kuwa na uwezo mdogo, lakini wana moyo mkuu katika kuheshimu maagizo ya Bwana na huisikiliza sauti ya Bwana kwa unyenyekevu.
Papa aliendelea kueleza kwamba katika taifa hili la Mungu , kila mtu ana nafasi yake. Na Bwana huongea na watu wake, kila mmoja katika nafsi yake na si katika wingi wao, kama ilivyo katika mkutano wa hadhara.
Na waamini wote , kwa ubatizo wao wamechaguliwa na Bwana. Bwana amechagua kila mmoja wao na kumpa jina na anamlinda. Bwana hutenda kinyume na Binadamu ambaye hutazama yaliyo ya nje na kuyatukuza, lakini Bwana hutazama ya ndani na kuyatukuza. Mara nyingi huchagua walio dhaifu katika jamii na kuwapa ukuu. Papa alieleza na kutoa mfano wa Daudi aliyekuwa mtoto wa mwisho ambaye kwa baba yake na ndugu zake alionekana kuwa hafai kitu.
Daudi hata pale allipoanguka katika dhambi, Bwana hakumwacha lakini alimsamehe na kuendelea kumpenda licha ya dhaifu huo, nae Daudi kwa unyenyekevu alitubu dhambi zake akisema, . Bwana mimi ni mkosaji.
Papa alieleza pia jinsi uaminifu wa Mkristu unavyotakiwa kutunza unyenyekevu na utii katika kuwasiliana na Bwana, akisema, tunapaswa kufurahia unyonge wetu, maana soni, unyenyekevu, na upole , ni muhimu sana katika maisha ya kikristo, kwa sababu, bwana anapenda kuwatazama walioa wadogo. Ni siku zote katika hali ya udhaifu na unyonge wetu kwende mbele ya ukuu wa Bwana na kuzungumza nae.
Papa alikamilisha homilia yake kwa kuomba maombezi ya Mtakatifu David - pia Bikira Maria, Mama wa upole na unyenyekevu, watuwaidie kujenga mahusiano ya karibu na Bwana katika hali ya unyenyekevu na upole.








All the contents on this site are copyrighted ©.