Sheria za nchi zisingatie pia utu, heshima na utamaduni wa kiafrika!
Wananchi wengi nchini Nigeria wanampongeza Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria kwa kupitisha
muswada wa sheria unaopiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja nchini Nigeria kwani
vitendo hivi ni kinyume cha utu, heshima na utamaduni wa kiafrika.
Wananchi
wanampongeza Rais kwa kuonesha msimamo dhidi ya kampeni za wanaharakati wanaotaka
kutumia mgongo wa demokrasia na uhuru usiokuwa na mipaka kuhalalisha matendo ambayo
yanakwenda kinyume cha utu na heshima ya binadamu. Hadi sasa kuna nchi 38 Barani Afrika
ambazo zinapiga rufuku ndoa za watu wa jinsia moja. Baadhi ya nchi kama vile Mauritania,
Sudan Kongwe na Uganda, watuhumiwa wanapokamatwa wanaweza kupata adhabu ya kifo.
Wakati
huo huo, Rais Yower Kaguta Museveni wa Uganda baada ya kupata shinikizo kutoka kwa
wanaharakati na baadhi ya Nchi za Ulaya kwa kutishia kusitisha kutoa misaada kwa Uganda,
Rais Museveni ameamua kuurudisha muswada wa sheria bungeni ili uweze kujadiliwa tena!
Muswada wa sheria Uganda ulikuwa unataka washitakiwa watakaotiwa hatiani wapewe adhabu
ya kifungo cha maisha jela.