Rais Jakaya Mrisho Kikwete amepangua Baraza la Mawaziri kwa kuwatema Mawaziri 5 katika
orodha mpya. Mawaziri 3 wamepandishwa cheo na wengine 10 ni sura mpya katika Baraza
la Mawaziri Tanzania. Dr. Asha-Rose Migiro ameteuliwa kuwa ni Waziri wa Katiba na
Sheria. Bi Saada Mkuya Salum ameteuliwa kuongoza Wizara ya Fedha.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua
baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-
1.0 OFISI
YA RAIS
Hakuna mabadiliko.
2.0 OFISI YA MAKAMU WA
RAIS
2.1 Waziri wa Nchi (Muungano) - Hakuna mabadiliko
2.2 Mhe.
Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb) Waziri wa Nchi (Mazingira).
2.3
Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb) Naibu Waziri
3.0
OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko
4.0
WIZARA
4.1 WIZARA YA FEDHA
4.1.1
Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu
Lameck NCHEMBA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha 4.1.2 Mhe.
Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha
4.2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna
mabadiliko
4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
4.3.1
Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba
na Sheria
4.3.2 Naibu Waziri - Hakuna mabadiliko
4.4
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko
4.5 WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
4.5.1 Waziri
- Hakuna mabadiliko
4.5.2 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
4.6 WIZARA YA
ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
(Mb) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
4.7 WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko
4.8 WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
4.8.1 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani
4.8.2 Naibu Waziri - Hakuna
Mabadiliko
4.9 WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
4.9.1
Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.9.2
Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii
4.10 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
4.10.1
Waziri: Hakuna mabadiliko
4.10.2 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
14.11 WIZARA YA MAENDELEO
YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
14.11.1 Waziri: Hakuna mabadiliko
14.
11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto
14.12 WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
14.12.1
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi
14.12.2 Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb) Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.13 WIZARA YA KAZI NA
AJIRA
Hakuna mabadiliko
14.14 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko 14.15
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
14.15.1 Waziri - Hakuna
mabadiliko
14.15.2 Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
14.16 WIZARA
YA MAJI
14.16.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
14.16.2 Mhe. Amos Gabriel
MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji
14.17 WIZARA YA KILIMO,
CHAKULA NA USHIRIKA
14.17.1 Waziri - Hakuna mabadiliko
14.17.2 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula
na Ushirika
4.18 WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna
mabadiliko
4.19 WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
4.19.1
Waziri - Hakuna mabadiliko
4.19.2 Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
4.20 WIZARA
YA MALIASILI NA UTALII
4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii
4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
4.21 WIZARA YA NISHATI NA MADINI
4.21.1
Waziri - Hakuna mabadiliko
4.21.2 Naibu Waziri (Madini) - Hakuna mabadiliko
4.21.3
Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)
Itakumbukwa
kwamba: Rais Jakaya Kikwete, kwa kutangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri
inafuatia uteuzi wa mawaziri watatu kutenguliwa, mmoja kujiuzulu na mwingine kufariki
dunia. Desemba 20, 2013. Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliwasilisha
bungeni taarifa ya uchunguzi kuhusiana na athari zilizojitokeza katika Operesheni
Tomokeza Ujangili iliyositishwa na serikali wakati wa Mkutano wa 13 wa Bunge kufuatilia
malalamiko ya wananchi, wabunge na wadau.
Akiwasilisha ripoti hiyo, Mwenyekiti
wa kamati hiyo, James Lembeli, alisema uchunguzi wao ulibaini kuwa operesheni hiyo
iliendeshwa bila kufuata taratibu na matokeo yake kusababisha mateso kwa raia, vifo
na upotevu wa mali hususani mifugo. Baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa, wabunge walichachamaa
na kushinikiza mawaziri ambao wizara zao zilihusika katika utekelezaji wa operesheni
hiyo wawajibike kisiasa au wawajibishwe.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,
Balozi Khamis Kagasheki, aliamua kujiuzulu wakati mjadala ukiendelea na siku hiyo
baadaye Rais Kikwete, alikubaliana na mapendekezo ya wabunge kwa kutengua uteuzi wa
mawaziri watatu, Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi); Mathayo David Mathayo
(Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na JKT). Januari Mosi,
2014, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alifariki dunia wakati akipatiwa
matibabu katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic, Pretoria, Afrika Kusini na kuzikwa
kijijini kwake Magunga, Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa tarehe 6 Januari 2014.
MABADILIKO
YA KWANZA
Rais Kikwete aliunda upya baraza lake la mawaziri Februari, 2008
baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu kutokana na kuhusishwa na
kashfa ya kuipa Kampuni ya Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas nchini
Marekani zabuni ya kufua umeme wa dharura wa megawati 100 kwa upendeleo. Lowassa alijiuzulu
sambamba na waliokuwa mawaziri wawili Dk. Ibrahim Msabaha (Ushirikiano wa Afrika Mashariki)
na Nazir Karamagi (Nishati na Madini). Karamagi na Dk. Msabaha, wote walikuwa wameiongoza
wizara ya Nishati na madini kwa nyakati tofauti.
Hatua ya kujiuzulu kwa Lowassa
na wenzake, ilitokana na ripoti ya Kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa
Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, iliyowasilishwa bungeni baada ya kukamilisha kazi ya
uchunguzi kujiridhisha kuhusiana na uhalali wa kampuni hiyo ndani na nje ya nchi.
Kamati hiyo pia iliundwa na Stella Manyanya (Viti Maalum), Mohamed Mnyaa (Mkanyageni-CUF),
aliyekuwa Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM) na Herbert Mntangi (Muheza-CCM), ambao
wal; ibaini kuwa kampuni hiyo ilikuwa feki.
MABADILIKO YA PILI Rais Kikwete
alifanya mabadiliko ya pili katika baraza lake Mei, 2008 baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa
Waziri wa Miundombinu na Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge. Chenge alichukua uamuzi
huo baada ya kubainika kuwa anamiliki akaunti iliyokuwa na Dola za Marekani milioni
moja (wakati huo Sh. bilioni 1.2) katika benki moja katika kisiwa New Jersey, nchini
Uingereza. Akaunti hiyo ilibainiwa na wapelelezi wa Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya
Ufisadi ya Uingereza (SFO) na kuhusishwa na fedha za kashfa ya ununuzi wa rada ya
kijeshi ambayo Tanzania iliinunua kutoka Uingereza wakati huo Chenge akiwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali mapema miaka ya 2000. Ilidaiwa kuwa huenda Chenge alipata fedha hizo
kutokana na rada hiyo kununuliwa kwa bei ya juu kuliko thamani yake. Baada ya Chenge
kujiuzulu, nafasi yake ilichukuliwa na Mbunge wa Bagamoyo, Dk. Kawambwa huku Rais
Kikwete pia akibadilisha mawaziri kadhaa.
MABADILIKO YA TATU
Mei 2012,
Rais Kikwete alifanya mabadiliko ya tatu katika baraza lake la mawaziri baada ya kuwaondoa
mawaziri sita kufuatia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG),
na kubaini mawaziri hao kwa nyakati tofauti walikiuka maadili ya utumishi wa umma
na kushindwa kuwajibika kisiasa kusimamia mali za umma. Katika mabadiliko hayo, waliondolewa
ni wa Mustafa Mkulo (Fedha); William Ngeleja (Nishati na Madini); Hadji Mponda (Afya
na Ustawi wa Jamii); Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii); Omari Nundu (Uchukuzi) na
Dk. Cyril Chami (Viwanda na Biashara). Wengine waliotimuliwa ni Naibu Waziri wa Uchukuzi,
Dk. Athumani Mfutakamba na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Lucy Nkya. Dk.
Mponda na Dk. Nkya waliponzwa na mgomo wa madaktari.