2014-01-18 12:22:25

Tume ya uchunguzi kuhusu Bikira Maria kutokea Medjugorje yakamilisha kazi yake


Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican amethibitisha kwamba, Tume ya uchunguzi iliyoundwa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kunako Mwaka 2010 kuchunguza ukweli kuhusu madai ya Bikira Maria kutokea huko Medjugorje umemaliza kazi yake, hapo tarehe 17 Januari 2014.

Taarifa imewasilishwa kwenye Baraza la Kipapa kwa ajili ya uamuzi zaidi. Itakumbukwa kwamba, Tume hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Kardinali Camilo Ruini, aliyewahi kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia na Makamu Askofu Jimbo kuu la Roma.

Kunako tarehe 21 Juni 1981 watoto kutoka Bosnia walidai kwamba, wametokewa na Bikira Maria. Tangu wakati huo, kumekuwepo na makundi makubwa ya waamini wanaotembelea na kusali katika eneo hili. Kwa miaka kadhaa Kanisa lilibaki kimya, lakini Mwaka 2010 Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa likaunda Tume maalum ili kuchunguza ukweli wa mambo!







All the contents on this site are copyrighted ©.