Tarehe 16 Januari 2014 Kanisa Katoliki nchini Italia linaadhimisha Siku ya 18 ya Mwendelezo
wa Majadiliano kati ya Wakristo na Wayahudi. Rabbi Abraham Skorka, Gombera wa Seminari
kuu ya Marabbi wa Amerika ya Kusini, ameandaa mkutano unaofanyika kwenye Chuo Kikuu
cha Kipapa cha Gregoriani, kilichoko hapa mjini Roma.
Itakumbukwa kwamba,
Rabbi Skorka kutoka Buonos Aires ni mwandishi mwenza na Baba Mtakatifu Francis. Wao
waliandika kitabu kinachojulikana kama "El cielo y la terra" "Mbingu na Dunia", ambacho
ni mkusanyo wa tema mbali mbali zinazohusu tunu msingi za maisha ya binadamu, maadili
na utu wema.
Mkutano huu unaangalia pamoja na mambo mengine: Majadiliano ya
Kidini kati ya Wayahudi na Wakatoliki, Miaka 50 Baada ya Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican
kuchapisha Hati ya Majadiliano ya Kidini, inayojulikana kwa Lugha ya Kilatini, "Nostra
Aetate", Mwelekeo kutoka Amerika ya Kusini. Kardinali Kurt Koch, Rais wa Tume ya Kipapa
ya uhusiano na Wayahudi.