2014-01-13 08:11:21

Orodha ya Makardinali wapya, 19; kati yao 16 wana haki ya kupiga na kupigiwa kura! Makardinali wateule 2 ni kutoka Afrika!


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili ya Ubatizo wa Bwana, tarehe 12 Januari 2014, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican alitangaza kwamba, katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Ukulu wa Mtakatifu Petro hapo tarehe 22 Februari 2014 atawasimika rasmi Makardinali kumi na sita wanaotoka katika nchi kumi na mbili dunini, kielelezo cha umoja na mshikamano wa dhati kati ya Makanisa mahalia na Kanisa la Roma.

Tarehe 23 Februari, Baba Mtakatifu ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu na Makardinali wapya. Tarehe 20 hadi tarehe 21 Februari, 2014, Baba Mtakatifu atakutanika na Makardinali wote ili kufanya tafakari ya kina kuhusu Familia.

Ifuatayo ni Orodha ya Makardinali Wapya 16 wenye haki ya kupiga na kupigiwa kura wakati wa uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Kuna Makardinali wengine 3 walioteuliwa kutokana na huduma iliyotukuka ndani ya Kanisa. Kumbe, jumla ya Makardinali wote ni 19 kutoka katika nchi kumi na tano duniani kote.

    Askofu mkuu Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican
    Askofu mkuu Lorenzo Baldisseri, Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu.
    Askofu mkuu Gerhard Ludwig Műller, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya mafundisho tanzu ya Kanisa
    Askofu mkuu Beniamino Stella,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makleri.
    Askofu mkuu Vincent Nichols, Jimbo kuu la Westminster, Uingereza.
    Askofu mkuu Leopoldo José Brenes Solórzano, Jimbo kuu la Managua (Nicaragua).
    Askofu mkuu Gérald Cyprien Lacroix, Jimbo kuu la Québec (Canada).
    Askofu mkuu Jean-Pierre Kutwa, Jimbo kuu la Abidjan (Pwani ya Pembe).
    Askofu mkuu Orani João Tempesta, Jimbo kuu la Rio de Janeiro (Brazil).

10. Askofu mkuu Gualtiero Bassetti, Jimbo kuu la Perugia-Città della Pieve (Italia).
11. Askofu mkuu Mario Aurelio Poli, Jimbo kuu la Buenos Aires (Argentina).
12. Askofu mkuu Andrew Yeom Soo Jung, Jimbo kuu la Seoul (Korea).
13. Askofu mkuu Ricardo Ezzati Andrello, S.D.B., Jimbo kuu la Santiago del Cile (Cile).
14. Askofu mkuu Philippe Nakellentuba Ouédraogo, Jimbo kuu la Ouagadougou (Burkina Faso).
15. Askofu mkuu Orlando B. Quevedo, O.M.I., Jimbo kuu la Cotabato (Filippine).
16. Askofu Chibly Langlois, Jimbo la Les Cayes (Haïti).

Baba Mtakatifu Francisko amewateuwa Maaskofu wengine watatu kutoka na utume wao uliotukuka kwa Kanisa. Hawa ni:


    Askofu mkuu mstaafu Loris Francesco Capovilla,wa Jimbo kuu la Mesembria.
    Askofu mkuu mstaafu Fernando Sebastián Aguilar, C.M.F., Jimbo kuu la Pamplona.
    Askofu mkuu mstaafu Kelvin Edward Felix, Jimbo kuu la Castries.









All the contents on this site are copyrighted ©.