2014-01-09 08:26:48

Rais wa Ufaransa kukutana na Papa Francisko mjini Vatican hapo tarehe 24 Januari 2014


Rais Francois Hollande wa Ufaransa anatarajiwa kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko hapo tarehe 24 Januari 2014, kadiri ya taarifa za vyombo vya habari kutoka Ufaransa. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Hollande kutembelea mjini Vatican baada ya kuchaguliwa kuwa ni Rais wa Ufaransa kunako Mei 2012.

Habari hizi, zimethibitishwa baadaye na Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican, alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mjini Vatican siku ya Alhamisi, tarehe 9 Januari 2014.

Kati ya maswala tete yanayouandama uongozi wa Rais Hollande ni uhalalishaji wa ndoa za watu wa jinsia moja na mchakato wa kutaka kuhalalisha kifo laini, mambo ambayo kadiri ya Mafundisho Jamii ya Kanisa yanasigana na utu pamoja na heshima ya binadamu.







All the contents on this site are copyrighted ©.