2014-01-09 15:00:23

Papa kutembelea Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu- Roma


Papa Francisko, Jumapili ya Januari 19, 2014 , nyakati za mchana, ana mpango wa kutembelea Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, iliyoko katika eneo la Castro Pretorio hapa Roma, karibu na kituo kikuu cha Treni cha mjini Roma. Akiwa katika Parokia hiyo, inayoongozwa na Wamisionari Wasalesian, Papa ataongoza Ibada ya Misa.
Kanisa hilo la moyo Mtakatifu wa Yesu lililojengwa na Mtakatifu John Bosco kwa niaba ya Papa Leo XIII , kwa ukarimu wa michango ya waamini wa Kanisa Katoliki, liliwekwa wakfu na Vika wa wakati ule Kardinali Lucido Parocchi Mei 14, 1887. Na Papa Benedict XV, 11februari, 1921, aliliinua katika heshima ya Basilica ndogo.
Hii ni Parokia ya nne kutembelewa na Papa Francisko tangu awe Askofu wa Jimbo la Roma, mwezi March mwaka jana. Alikwisha tembelea Kanisa la Watakatifu Elizabeth na Zakaria Mei 26 , na Desemba 1 alitembelea Parokia ya Mtakatifu Cyril wa Alexandria na Januari 6 katika Kanisa Mtakatifu Alfonsi Maria de ' Liguori,ikiwa ni ziara ya faragha kwa ajili ya kujionea pango hai katika mazingira halisi ya wakati wa kzaliwa Yesu Bethlehem.








All the contents on this site are copyrighted ©.