Papa amsalimia Padre mzee kuliko wote Italia - Vatican
Jumatano baada ya katekesi yake kwa mahujaji na wageni, Papa Francisko, akiwa katika
uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, alisalimiana na Padre Don Alessandro De
Sanctis , mwenye umri wa miaka 95 ya kuzaliwa na miaka 72 ya Upadre , anayeaminika
kuwa ni Padre Mzee kuliko Mapadre wote wa Italia. Padre Alessandro de Sanctis ni
Paroko wa Parokia ya Filey Frusinate . Wakisalimiana, Papa Francisko alimtania
Don Alessandro ambaye kwa kumtazama haonyeshi kuwa na umri mkubwa kiasi hicho, kwa
kumwambia umeificha wapi miaka hii yote 95, naye Padre alijibu , Mtu Mtakatifu niombee,
kumpatia Papa, barua iliyoandikwa kwa mkono wake mwenyewe na kalamu ya zamani ya
wino. Akizungumza na wanahabari baada ya kukutana na Papa , Don Alessandro alieleza
kwamba , alikuwa na wasiwasi moyoni kwamba Papa ataondoka mahali hapo bila kumfikia
na hivyo alianza kukata tamaa na hata haikuona tena maana ya kuandika barua hiyo
kwa Papa. Kimyakimya alisali ili Bwana amjalie neema ya kutoa mkono wake wa tisa kwa
Papa, katika maisha yake. Na Bwana aliitikia Ombi lake . Na alionyesha kushangazwa
na unyenyekevu wa Papa Francisko katika kukutana na watu , akisema kweli ni jambo
jipya linalo vutia wengi.