Kazi ya Uinjilishaji ni wajibu wa Kanisa zima na watu wote wa Mungu .Hivyo Wakritu
wote wameitwa kufanikisha utume huu wa kanisa. Papa Francisko ameandika katika ujumbe
wake kwa ajili ya Mkutano wa Kitaifa wa 13, unaokutanisha jumuiya zote msingi mahalia
za Kikanisa nchini Brazil. Mkutano huo ulianza Jumanne mjini Juazeito de Norte
, ukiongozwa na Mada Kuu "Haki na Unabii katika huduma ya maisha ", na unakamilika
tarehe 11 Januari . Katika ujumbe huo, Papa amesisitiza kwamba, waamini wote wanapaswa
kutembelea maeneo yote ya vijijini na mijini pia, kuipeleka furaha ya Injili, kwa
kila binadamu, mwanamme na mwanamke . Papa, amewakabidhi washiriki wa mkutano
huo katika ulinzi wa Mama yetu wa Aparecida ,huku akisistiza kwamba, Jumuiya msingi
mahalia , ni muhimu katika kazi msingi za Utume wa Kanisa. Na kwamba, Mara nyingi
, kama alivyoeleza katika waraka wake wa Evangelii Gaudium, katika himizo jipya la
Kuinjilisha, na juu ya uwezo wa mazungumzano na ulimwengu katika kulifanya upya Kanisa.
Na pia kama alivyoonya katika waraka wake wa kwanza wa kitume wenye kuwa na
utajiri mkubwa wa ushauri, kwamba, jumuiya msingi mahalia hazipaswi kupoteza mahusiano
yake na utajiri wa parokia mahalia , ambazo huchanganyika na vyombo vya kichungaji
vya kanisa kwa namna ya kipekee.
Mwisho Papa ametoa wito kwa washiriki wa
Mkutano kwa onyo la Mtume Paulo kwa Wakoritho: " Ole wangu kama sitaihubiri injili.