Mapigano ya Kikabila nchini Nigeria yasababisha vifo vya watu zaidi ya 40
Mapema juma hili watu zaidi ya arobaini wameuwawa kikatiliki, wengi wao wakiwa ni
wanawake na watoto huko Plateau na Kaduna, nchini Nigeria. Taarifa zinaonesha kwamba,
haya ni mapigano ya kikabila yanayoendeshwa na Kabila la Fulani. Mapigano hayo yamepelekea
nyumba na mifugo kadhaa kuchomwa moto!
Taarifa inaonesha kwamba, askari wanne
waliokuwa wanarudi makwao baada ya kumaliza zamu yao ya ulinzi kwenye Benki Wilayani
Rigasa walivamiwa na kuuwawa kikatili. Wachunguzi wa mambo wanasema, haya ni mapigano
kati ya wafugaji wanaotafuta maeneo ya kulishia na kunywesha mifugo yao pamoja na
wakulima wanaotafuta maeneo mazuri zaidi ya kilimo.
Mapigano kati ya kabila
la Wafulani na Watarok, katika kipindi cha kuanzia mwaka 1992 hadi Mwaka 2013 yamesababisha
zaidi ya wananchi elfu kumi kuuwawa kikatili huko Plateau na Kaduna, Nigeria.