2014-01-08 16:08:23

Kuweni macho na Manabii wa uongo - Papa


Mkristu wa kweli anajua jinsi ya kulinda moyo wake,na huweza kutofautisha yatokayo kwa Mungu na yatokayo kwa manabii wa uongo. Ni ujumbe wa Papa Francisko wakati wa Ibada ya Misa ya ya Asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta, siku ya Jumanne. Katika homilia yake Papa alieleza kuwa, njia ya Yesu ni ile ya kuhudumia kwa unyenyekevu, njia ambayo Wakristo wote wameitwa kuifuata.Alieleza hilo akinukuu barua ya kwanza ya Mtume Yohane , ambamo anasema "Kaeni katika Bwana.
Papa aliendelea kufaafanua maneno hayo akisema, ni ushauri katika kuifuata njia ya maisha, uliotolewa na Mtume Yohane, ambao huurudia mara kwa mara tena kwa uthabiti zaidi .Mtume Yohane anaonyesha moja ya mitazamo ya Mkristo anayetaka kubaki katika Bwana, kwamba ni kuelewa nini kinatokea katika moyo wake mwenyewe. Na kwa sababu hiyo anaonya si kila roho ni roho wa imani , kwa kuwa pia kuna roho za majaribu na maovu . Na hivyo , ni vyema kujua na kuzitambua roho bandia na roho wa kweli anayetusaidia kubaki katika Bwana."
Aliongeza , Mioyo yetu daima ina hamu ya kuepnda na pia huwaza. Na hivyo ni muhimu daima kutafakari kwa kina yapi yanatoka kwa Bwana na yapi yanatuweka mbali na Bwana. Na hii ndiyo sababu Mtume Yohana, anatusihi kuwa makini katika mtihani huu wa majaribu. Katika yale tunayo yafikiri na yale tunayo yatamani.
Kwa muono huo, Papa ametoa mwaliko kwa watu wote kufikiri vyema hasa kinanachosikika ndani ya moyo wenyewe . Yale tunayo yafikiri na kuhisi na yale tunayo tamani na vile tunavyohitaji, tunapaswa kuchunguza kwa kina kama kweli ndiyo uchaguzi wa roho, au tunapapukia tu kukubali bila utambuzi.

Papa alimalizia akisema, mara nyingi, mioyo yetu ni sawa na barabara , kila kitu hupita huko ... Hutuweka katika mtihani wa kuchagua yanayotoka kwa Mungu na yasiyotoka kwa kwa Mungu . Na iwapo kinatambua kigezo cha kweli kinacho ongoza katika kupambanua mawazo na tamaa za uongo. Papa amekitaja kigezo hicho kuwa ni Neno aliyemwilishwa. Neno wa Mungu aliyekuja katika mwili , na kukaa kwetu ambaye ni Yesu Kristo! Yesu Kristo ambaye alifanya mtu, Mungu aliyejishusha mwenyewe katika unyenyekevu wa upendo , kwa ajili kututumikia sisi sote. Papa alieleza na kuomba Mtume Yohana utupe neema hii ya kujua kile kinachotokea katika mioyo yetu, na kuwa na hekima ya kutambua kile ambacho ni cha Mungu na visivyo toka kwa Mungu".








All the contents on this site are copyrighted ©.