2014-01-08 09:04:32

Cheo cha Monsinyori kutolewa baada ya umri wa miaka 65-Vatican


Sekretarieti ya Jimbo la Takatifu , Jumanne ilitoa tamko linaloonyesha mabadiliko yaliyofanywa na Papa Francisko katika utoaji wa cheo cha Monsinyori. Katika barua iliyopelekwa katika ofisi zote za uwakilishi na wajumbe wa Papa duniani kote, (Nunciatures) , pia kwa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki kwamba, katika majimbo yote duniani, cheo hicho cha heshima pekee cha Kikanisa, tangu sasa katika maana hiyo ya Monsinyori itakuwa sawa na “Kasisi wa Kipapa “. Na kwamba cheo hicho kitatolewa tu kwa Mapadre waliofikisha umri wa miaka 65.
Pia Barua hiyo, inatoa ufafanuzi zaidi juu ya matumizi ya cheo hiki cha monsinyori , katika baadhi ya ofisi muhimu za Kanisa, - ambapo matumizi ya jina Monsinyori limekuwa ni mila na desturi , kwa mfano katika ofisi ya Askofu, au Mwakilishi Mkuu wa Jimbo au Vika wa jimbo , katika hilo bado hakuna mabadiliko, kama ilivyo pia katika walio kabidhiwa dhamana ya huduma na kazi katika Ofisi za Curia ya Roma, Na Pia barua inaweka wazi kwamba wale wote ambao tayari wamekwisha pewa jina hilo rasmi wataendelea kulitumia .Na pia tamko jipya halifanyi mabadiliko kwa walei waliotunukiwa heshima hiyo na Papa .
Mwisho barua hiyo , inasema, Papa Paulo VI, mwaka 1968, alipunguza wingi wa watu waliokuwa wakitumia jina la cheo hiki cha heshima katika Kanisa. Na hivyo maamuzi ya Papa Francisko yako katika muono huohuo wa ndani , watumishi wa kanisa kubaki watu wa kawaida.







All the contents on this site are copyrighted ©.