2014-01-02 10:02:08

Papa atembelea na kusali kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu, mjini Roma!


Baba Mtakatifu Francisko katika Maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu, iliyoadhimishwa hapo tarehe Mosi, Januari 2014, jioni alikwenda kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu lililoko mjini Roma na kusali huko kwa kitambo, mbele ya Sanamu ya Bikira Maria Mama wa Mungu.

Katika mahubiri yake wakati wa Maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu alifanya rejea kuhusu Kanisa kuu la Bikira Maria Mkuu pamoja na Sanamu ya Bikira Maria Mama wa Mungu inayoheshimiwa na waamini.

Itakumbukwa kwamba, Baba Mtakatifu Francisko ana ibada ya pekee kwa Bikira Maria na mara kadhaa baada ya matukio makuu katika maisha na utume wa Kanisa amekuwa akienda kusali kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu.

Ndani ya Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu, vijana na watalii wengi walishikwa na bumbuwazi walipokutana uso kwa uso na Baba Mtakatifu Francisko na kusalimiana naye! Mtu wa watu hana makuu!







All the contents on this site are copyrighted ©.