2014-01-01 08:35:50

Hatimaye, Padre Vandenbeusch aachiwa huru!


Padre Georges Vandenbeusch, mwenye umri wa miaka 42 aliyekuwa ametekwa nyara na watu waliokuwa na silaha hapo tarehe 14 Novemba 2013 wakati akitoa huduma kwenye Parokia ya Nguetchewe, Kaskazini mwa Cameroon, ameachiliwa huru, mwishoni mwa mwaka 2013. Habari hizi zimethibitishwa na Rais Francois Hollande wa Ufaransa ambaye anasema kwamba, hali ya Padre Georges ni njema.

Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican amepokea habari hizi kwa moyo wa furaha na shukrani na anawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema kuendelea kusali na kuwaombea watu mbali mbali waliotekwa njara na hadi sasa hawajulikani mahali waliko.







All the contents on this site are copyrighted ©.