Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Bikira Maria Mama wa Mungu na Siku ya Kuombea
Amani Duniani kwa mwaka 2014
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe Mosi Januari 2014 anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya
Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa ajili ya Sherehe
ya Bikira Maria Mama wa Mungu. Hizi ni kati ya sherehe kubwa za Bikira Maria zinazoadhimishwa
na Kanisa katika Kipindi cha Mwaka sanjari na Siku ya Kuombea Amani Duniani.
Ujumbe
wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Mwaka 2014 unaongozwa na kauli mbiu "Udugu ni msingi
na njia ya amani" mafundisho msingi ya Kanisa kuhusu masuala ya kijamii, kama sehemu
ya mchakato wa kudumisha haki, amani na maendeleo endelevu.
Udugu ni jambo
muhimu sana katika mapambano dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi. Udugu unazima vita
na madhara yake; upambana kufa na kupona na rushwa, ufisadi na uhalifu wa makundi.
Udugu unalinda na kutunza mazingira.