Askofu Nunzio Galantino ateuliwa kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 28 Desemba 2013 amemteua Askofu Nunzio Galantino
kutoka Jimbo Katoliki la Cassano all'Jonio, Italia kuwa Katibu mkuu wa muda wa Baraza
Maaskofu Katoliki Italia.
Akizungumzia kuhusu uteuzi huu, Padre Federico Lombardi
msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Askofu Galantino ameteuliwa kuwa Katibu
mkuu kwa muda usiojulikana na ataendelea kutekeleza utume wake kama Askofu wa Jimbo
Katoliki Cassano. Lengo ni kuendeleza shughuli za Baraza la Maaskofu Katoliki Italia
na kwamba, muda mrefu itambidi kuwa mjini Roma.
Baba Mtakatifu Francisko ameandika
barua kwa Familia ya Mungu Jimbo Katoliki Cassano all'Jonio, Italia akiwatakia kheri
na baraka wakati huu wa kipindi cha Noeli na Mwaka mpya 2014. Anasema, anatarajia
siku moja, kuonana nao, ili waweze kufahamiana zaidi.
Kwa namna ya pekee,
anawaomba, waamini wa Jimbo hili kumruhusu Askofu Galantino kutekeleza dhamana yake
kama Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia. Anatambua usumbufu watakaokutana
nao kwa vile wanampenda sana Askofu wao, lakini anawaomba wamsamehe na kumruhusu Askofu
Galantino afanye utume huu mpya ambao ni sadaka kubwa, kwani itambidi asafiri mara
kwa mara na kwamba, anahitaji msaada wa sala zao katika hija hii ya imani!
Baba
Mtakatifu anawaalika waamini kufahamu kuhusu uteuzi huu na kuendelea kumwombea katika
maisha na utuke wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.