2013-12-28 14:05:15

Serikali ya Syria yatuma ujumbe kwa Papa Francisko na kuonesha msimamo wake!


Askofu mkuu Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, Jumamosi, tarehe 28 Desemba 2013 amekutana na ujumbe kutoka Serikali ya Syria, uliokuwa unaongozwa na Bwana Joseph Sweid, Waziri wa mambo ya nchi, aliyekuwa ameandamana na Bwana Hussam Eddin Aala, Naibu mkurugenzi mkuu masuala ya Ulaya, ambaye pia aliwahi kuwa Balozi wa Syria mjini Vatican.

Ujumbe huu pia umepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Viongozi kutoka Syria umewasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Assad wa Syria kwa Baba Mtakatifu Francisko na wameonesha msimamo wa Serikali ya Syria.

Haya yamebainishwa na Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.







All the contents on this site are copyrighted ©.