2013-12-28 10:38:20

Jeshi la Serikali ya Nigeria na Boko Haram bado wanapimana nguvu!


Katika mkesha wa Noeli kumekuwepo na mapambano makali kati ya Jeshi la Serikali ya Nigeria na Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram, ambacho kwa miaka minne, kimekuwa kikiendesha vitendo vya kigaidi nchini humo na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Mapambano ya silaha yamefanyika katika eneo ambalo limetangazwa kuwa ni la hatari, yaani kwenye Majimbo ya: Borno, Yobe na Adamawa. Serikali ya Rais Goodluck Jonathan imetangaza hali ya hatari Kaskazini mwa Nigeria hadi mwishoni mwa Mei, 2014.







All the contents on this site are copyrighted ©.