2013-12-27 12:53:05

Uwakilishi kutoka Parokia za Jimbo la Roma kuungana na Papa Francisko wakati wa Ibada za Misa za asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta


Inatazamiwa tangu, January 2014 , Maparoko wa Parokia mbalimbali za jimbo la Roma, watapewa taarifa kupitia Vika wa Jimbo la Roma, lini wanaweza kupeleka maombi ya kushiriki katika Ibada, zinazo ongozwa na Papa , katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta, ndani ya Vatican.

Kulingana na nafasi ya Kanisa, Maparoko wataandamana na kundi dogo la wanaparokia wapatao 25. Na kwa kuwa si rahisi Papa kupata muda wa kutembelea Parokia zote za Jimbo la Roma, ushiriki huu katika ibada za asubuhi, utawezesha wanaparokia mbalimbali kukutana na Askofu wao , walau kukiwa na nafasi mwakilishi mmoja kutoka kila Parokia.

Padre Fedrico Lombardi, Msemaji wa Vatican ,ameeleza kama kujibu makala iliyoandikwa katika gazeti la Corriere della Sera toleo la tarehe 24 .12 .13, iwapo makundi ya waamini wa Parokia za Jimbo la Rome wamealikwa kushiriki katika Ibada za Misa inayongozwa na Papa majira ya asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya vatican, amesema, hadi Sasa waliohudhuria katika ibada hizo ni makundi maalum ya wafanyakazi wa Vatican.









All the contents on this site are copyrighted ©.