Kardinali Ouellet asema, mwaka 2013 umekuwa ni mwaka wa kihistoria kwa Kanisa.
Katika mwaka huu tunao elekea kuufunga, kwa hakika umekuwa ni mwaka wa kipekee katika
maisha ya Kanisa, na hasa kwa tukio jipya la kihistoria la kustaafu katika kiti cha
Petro, Papa Benedikto XV1, na kuchaguliwa kwa mrithi wake Papa Francisko. Ni maoni
ya Kardinali Marc Ouellet , Mkuu Decania ya Maaskofu, wakati akihojiwa na Hèlène Destombes
wa Radio Vatican, juu ya kustaafu kwa Papa Benedikto XV1.
Kardinali Ouellet
analichukulia tukio la kujiuzuru kwa Papa Benedikto XV1, kuwa ni tukio kubwa jipya
katika historia ya kipindi kirefu kwa Kanisa. Kitendo kilicho shuhudia maana ya unyenyekevu
na imani kubwa kwa Roho Mtakatifu, kwa ajili ya utendaji wa siku za usoni kwa Kanisa.
Na hivyo tunapaswa kumshukuru Papa Benedikto XVI, kwa kufungua upya upeo wa macho,
na fursa ya kuchaguliwa kwa Papa mpya Francisko.
Kardinali anaamini kwamba,
kuna ni mwendelezo kwa yale yaliyoanzishwa na Papa Mstaafu Benedikto XVI, yanayo fanyiwa
kazi na Papa Francisko. Na hivyo kwa tathmini ya mwaka 2013, inaonyesha kwamba, ulikuwa
ni wakati wa mabadiliko makubwa katika historia ya Kanisa , katika mtazamo wa utendaji
wa kichungaji kwa maongozi ya Papa Francisko.
Kardinali ametaja mageuzi hasa
katika maisha ya Kiinjili, ambamo Papa Francisko, amekuwa akisisitiza mawasiliano
mpya ya muumini kujiweka karibu zaidi na Mungu, bila ya kujali hali yao au itifaki
yao, wote anawahimiza kumgeukia Mungu kama jambo la dharura. Na katika kufanya hivyo
, anamtaka kila Askofu awe mchungaji mwema, wote kuwa wa mchungaji mwema, anayekaa
daima karibu na wanakondoo wake, akiwachunga kwa moyo wa upendo mkuu na huruma ,
na akiwajaza zawadi ya faraja na matumaini mapya.
Na kwamba, katika mwaka huu
2013, katika mtazamo wa Papa Francisko, umetoa msisitizo mkubwa katika kujali maisha
ya umma mzima wa dunia. Na huu ni mfumo mpya wa ajabu katika uinjilishaji. Papa amekuwa
ni ishara ya ushawishi, katika hitaji la watu kujenga matumaini katika ubinadamu
na kwamba Mungu hupatikana katika sura ya binadamu hasa mtu maskini na mnyonge. Hii
ni habari njema kwa watu wote! tunapaswa kupokea ujumbe huo na kuufurahia.