Mwenyezi Mungu ulilisahau Bara la Afrika na Watu wake!
Baba Mtakatifu Francisko katika salam zake za Noeli kwa Mji wa Roma na Ulimwengu kwa
ujumla, "Urbi et Orbi" amelikumbuka Bara la Afrika kwa namna ya pekee na kumwomba
Yesu Mfalme wa Amani, kutolisahau wala kusahau mahangaiko ya wananchi wa Bara la Afrika.
Baba
Mtakatifu amesali kwa ajili ya Nigeria ambako watu wasiokuwa na hatia wanaendelea
kuteseka na kudhulumiwa. Amewakumbuka wale wote wanaoteseka kutokana na imani yao
kwa Kristo na Kanisa lake. Katika sala zake, Baba Mtakatifu anaendelea kuwakumbuka
wahamiaji, wakimbizi na watu wasiokuwa na makazi; hasa wale wanaoishi kwenye Kona
ya Pembe ya Afrika na DRC.
Baba Mtakatifu anamwomba Mtoto Yesu asaidie mchakato
wa upatanisho nchini Sudan ya Kusini, ambako vita na kinzani za kijamii zimekwisha
sababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Vita anasema Baba Mtakatifu Francisko
nchini Sudan ya Kusini inatishia amani, usalama na utulivu kati ya watu!