Katika adhimisho ya Siku Kuu ya Mtakatifu Stefano, Papa ahimiza kuwaombea wanaobaguliwa
kidini.
Mama Kanisa akiadhimisha la Siku Kuu ya Mtakatifu Stefano, ambayo kijamii hujulikana
kama "Boxing Day "Baba Mtakatifu Francisko, nyakati za adhuhuri kabla ya sala ya Malaika
wa Bwana, aliwahutubia mahujaji na wageni waliokusanyika katika uwanja wa kanisa kuu
wa Mtakatifu Petro. Katika hotuba hiyo alieleza kuwa, maadhimisho ya Siku Kuu
ya Noel, kiliturujia huendelezwa kwa muda wa siku nane. Na ni wakati wa furaha kubwa
kwa watu wote wa Mungu ! Katika mwendelezo wa furaha hiyo, baada ya Siku Kuu ya kuzaliwa
Kristu , Kiliturujia hufuatia Siku Kuu ya Mtakatifu Stefano , kama sehemu ya sikukuu
hiyo. Mtakatifu Stefano , NI shahidi mfiadini wa kwanza wa Kanisa. Habari zake zimeandikwa
katika Kitabu cha Matendo Mitume... Mtakatifu Stephano alikuwa ni mtu aliyejaa
imani na Roho Mtakatifu" ( 06:05 ). Pamoja nae pia waliteuliwa wengine sita kwa ajili
ya kuhudumia wajane na maskini katika kanisa la kwanza wa Yerusalemu. Na aliuawa
kwa kupigwa mawe nje ya ukuta wa mji wa Yesusalem. Papa amekifananisha kifo cha Stefano
na kifo cha Yesu, kwamba wote waliowaombea msamaha wauaji wao.
Katika maelezo
yake Papa amefafanua kwa nini Kanisa lina adhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Sptefano,
ambayo kwa mtazamo wa haraka haraka mtu anapata fikira kama iko nje ya kipindi hiki
cha kufurahia kuzaliwa kwa Bwana. Lakini kumbe katika kina cha imani, inahusiana na
mwendeleo wa maisha. Amesema, Noel ni sherehe ya maisha mapya yenye kutupa hisia
ya utulivu na amani , si kipindi cha kufkiria fujo na ghasia za kutisha. Lakini
katika mtazamo wa mtazamo wa imani , Sikukuu ya Mtakatifu Stefano, ni mahali pake,
katika maana ya ndani ya Noel. kwa kuwa katika kifo chandaniya Kristu huzaliwa maisha
mapya. Katika vurugu mauaji hushindwa na hushindwa na upendo, na hivyo kifo hutoa
maisha. Kanisa linaona katika majitoleo ya sadaka ya mashahidi wafiadijni, huzaliwa
mbingu. Na hivyo kwa mtazamo huo, kumbe tunaisherhehea kuuawa kwa Mtakatifu Stefano
inakuw ani Siku yake ya kuzaliwa upya, katika Kristo.Yesu hukibadili kifo cha wale
wanaompenda na kumwamini kwa kuwapa maisha mapya. Katika mauaji ya Stefano, mnaonyesha
pia mapambano kati ya mema na mabaya, kati ya chuki na msamaha, kati ya upole na
vurugu , ambayo ni hali halisi zilivyo kuwa , wakati wa Kifo cha Yesu Msalabani. Na
hivyo kumbukumbu ya shahidi wa kwanza wa imani, hivyo, inafuta mara moja, sura ya
noel ya uongo, ambayo haimo katika Injili.
Liturujia ya leo, inaturudisha
katika maana ya kweli ya Umwilisho,inaunganisha Bethlehemu na Kalvari na kutukumbusha
kwamba, wokovu ya Mungu, ni mapambano dhidi ya dhambi, ni kupita katika mlango mwembamba
wa Msalaba. Hii ni njia ambayo Yesu aliweka wazi kwa wanafunzi wake , kama ilivyoshuhudiwa
na Injili ya leo:nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu . Lakini
atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa "(Mt 10:22).
Hivyo, Baba Mtakatifu
Francisko alihimiza kuomba hasa kwa ajili ya Wakristo , wanao baguliwa kwa sababu
ya ushuhuda wao kwa Kristo na Injili. Na kutoa mwaliko wa kuwa karibu na ndugu, wake
kwa waume, wale ambao, kama Mtakatifu Stefano, wanashutumiwa na kukabiliwa na unyanyasaji
wa aina mbalimbali. Na hii inatokea hasa pale ambako, uhuru wa dini bado si wa uhakika
au si kamilifu. Papa ameasa hili pia linaweza kutokea hata katika nchi zilizotia
sahihi katika hati ya makubaliano ya kulinda uhuru wa dhamiri, na haki za binadamu,
ambako waumini, na hasa Wakristo, bado wanakumbana na mapungufu katika uhuru wao
na ubaguzi. Kwa Wakristo, hii si ajabu, kwa sababu Yesu alitabiri hilo kama fursa
ya kuishuhudia imani. Papa aliomba msaada wa maombezi ya Mama Bikira Maria Malkia
wa Mashahidi atusaidie kukiishi kipindi hiki cha Noel, kwa mwamko wa imani na upendo
kwa kuangaziwa na Mtakatifu Stefano na mashahidi wafia dini wa Kanisa.
Baada
ya Sala ya Malaika wa Bwana, Papa alitoa salaam zake za matashi mema nabaraka kwa
makundi mbalimbali zikiwemo familia kutoka Parokia mbalimbali za jimbo la Roma, na
wale wote wanaofanya hija katika Pango la Noel, kumwona Mtoto Yesu, Maria na Yosef
, waweze kutoa ahadi ya ukarimu wa upendo kwa mtu mwingine, ili ndani ya familia
na jamii, watu waiishi hali ya hewa ya uelewa na udugu, kwa ajili ya manufaa ya wote.