2013-12-25 15:42:56

Ujumbe wa Papa wa Noel,wamtaka kila mtu kuwa mjenzi wa amani duniani.


Papa Francisko akifuata utaratibu wa watangulizi wake , katika kuadhimisha Sikuu ya Noel, Jumatano hii 25 Desemba, nyakati za adhuhuri, alitoa ujumbe wake kwa jiji na dunia kwa ujumla "Urbi et Orbi, mbele ya mahujaji na wageni walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Tukio lililopambwa na nyimbo za Kitaifa za Vatican na Italia, zilizotumbuizwa na bendi ya walinzi wa Vatican.
Ujumbe wa Papa ulianza na maneno ya kumtukuza Mungu kama ilivyoandikwa katika Injili ya Luka2:14; Utukufu kwa Mungu juu mbinguni ,na amani duniani kati ya wale alio waridhia.

Papa aliuangalisha ujumbe wake kwa wimbo wa Malaika waliowatokea wachungaji Bethlehem Usiku alio zaliwa Yesu Kristu, akisema, ni wimbo ambao unaunganisha mbinguni na duniani , kutoa sifa na utukufu mbinguni, na ahadi ya amani duniani na watu wake wote.

Papa alitoa wito kwa wote , kushiriki katika wimbo huu wa malaika, kila mtu mke kwa mme, kuwa macho na giza la dunia, kwa kila anaye tarajia ulimwengu bora, kuwajali wengine kwa unyenyekevu na mwenye kutafuta na kutimiza wajibu wake kwa ajili ya Utukufu wa Mungu ! Papa alifafanua, hilo ndilo tunalotakiwa kulifurahia katika Siku Kuu hii ya Noel.

Zaidi ya yote , kumtukuza Mungu , kwa kuwa yeye ni mwema, na mwaminifu na mwenye huruma. Papa alieleza na na kuonyesha tumaini lake kwamba, kila mtu ataweza kuujua uso wa kweli wa Mungu Baba, aliye tupatia mwanae Yesu Kristu. Papa aliendelea kuonyesha tumaini lake kwamba, kila mtu atajisikia kuwa karibu wa Mungu, kuishi na uwepo wake Mungu , kumpenda na kumwabudu. Na kila mmoja awe na muda wa kumtukuza Mungu na juu ya yote kwa maisha yake, na kwa ajili ya upendo kwa jirani na jamii yote ya wake kwa waume.

Papa aliendelea kuzungumzia amani kwa watu wote,akisema amani ya kweli si uwepo wa urari katika nguvu za upinzani. Na si kuwa na sura ya kinafiki yenye kupendeza kijuujuu lakini kumbe ndani yake mmefichika mizozo na migawanyiko.Papa aliitaja amani ya kweli yenye kuitikia wito na ahadi kuuishi amani kila siku, kama zawadi ya Mungu , kwa neema ya anayotupatia kupitia mwanae Yesu Kristo .

Alisema, kwa kumwangalia Mtoto horini, mawazo yetu yanarejea kwa watoto wale ambao ni waathirika wa vita , na pia tunawawazia wazee, na wanawake wanaodhulumika , wagonjwa na mahangaiko mengine yanayosababishwa navita vyenye kuharibu na kuangamiza maisha ya wengi !



Papa aliyakumbuka maisha wengi yanayoendelea kudharirishwa katika siku hizi , akivitaja vita vya Syria, vinavyochochewa na chuki na kisasi.
Kwa tafakari hiyo, Papa alitoa wito wa kuendelee kumwomba Bwana kwa ajili ya watu wapendwa Syria wanaoteseka, na ili Bwana awawezesha wahusika katika mgogoro huu,kukomesha vurugu zote na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya misaada ya kibinadamu.

Papa aliweka imani yake katika sala akisema, tumeona jinsi sala ilivyo na nguvu. Na alifurahia kwamba, kwamba wafuasi wa madhehebu mbalimbali ya dini, wameungana na Kanisa Katoliki katika kutolea maombi ya kuombea amani Syria. Papa alisihi hakuna kupoteza ujasiri wa maombi! Ujasiri wa kusema : Bwana , tupe zawadi ya amani yako kwa ajili ya Syria na kwa dunia nzima.

Papa aliendelea kumwomba Bwana , Zawadi ya amani pia kwa mataifa ya Afrika , hasa ambayo kwa wakati huu yako katika hali ya machafuko ya mara kwa mara , Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo mara nyingi imesahauli au kupuuzwa. Allikumbuka Nigeria , Mashariki mwa Congo, na Pembe ya Afrika somalia, Sudan Kusini ambako kunashuhudiwa maisha ya watu kuteketezwa na moyo wa chuki na fitina. Lakini Bwana , kamwe hamsahau mtu ! Amemsihi Mungu ayawezeshe mataifa hayo, kupata neema ya amani na watu kupata mahitaji yao ya kiroho na kiwmili katika hali ya amani na maridhiano.

Aliendelea kumlilia Mkuu wa Amani, afanye mageuzi katika mioyo ya watu iliyojaa vurugu na chuki, ili ihamasike kuweka silaha chini na kufuata njia ya mazungumzano katika kufuta tofauti zao.

Na aliomba zawadi ya matumaini na faraja kwa wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta maisha ya heshima na ahueni ili waweze kupokelewa vyema kule wanaokimbilia. Alieleza hilo kwa kukumbuka janga lililoshuhudiwa mwaka huu la vifo vingi vilivyo tokea Lampedusa, akiomba kamwe janga hilo lisitokee tena !

Vivyo hivyo aliwakumbuka kafara wote wa utumwa mambo leo, hasa wanajihusisha na usafirishwaji biandamu kinyume cha ubinadamu, ili wapate kutambua ukubwa wa uhalifu huu dhidi ya ubinadamu. Na pia aliangalisha kwa watoto wengi waliotekwa nyara, waliojeruhiwa na kuuawa katika vita vya silaha, na wale wote ambaohaki yao ya utoto wao imenyakuliwa na kulazimishwa kuingia katika majeshi .
Pia ameomba msaada na ulinzi kwa wahanga wa maafa asilia kama ilivyotokea huko Ufilipino , ambako kuna walioathirika na kimbunga kikali cha hivi karibuni.
Baada ya maelezo hayo , Papa aliweka matumaini yake yote kwa mwanga wa mtoto aliyezaliwa Bethlehemu, Mwokozi, Yesu Kristo Bwana, akisema, ebu na turuhusu mioyo yetu kuguswa ,na kuruhusu kuongozwa na moto wa upendo wa Mungu , Mungu ambaye yeye mwenyewe ndiye upendo kamili ambaye tunatolea sifa na utukufu kwake milele! Mungu ni amani.Na atusaidie kuleta amani kila siku, katika maisha yetu, katika familia zetu, katika miji na mataifa yetu , katika dunia nzima. Hebu na turuhusu sisi wenyewe kuongozwa na wema wa Mungu.

Baada ya ujumbe huu , Papa alikamilisha kwa kurejea adhimisho la Noeli akisema, , kwa mwanga wa Siku Kuu hii na tumaini la Injili , inayochipuka kutoka unyenyekevu imara wa Bethlehem, ninawatakia zawadi ya Krismasi yenye furaha na amani, hasa kwa watoto na wazee vijana na familia, maskini na wanyonge. Yesu, ambaye alizaliwa kwa ajili yetu, awe faraja kw awale wote walio katika taabu za ugonjwa na mateso mengine, na awadumishe wale wote walioyatolea maisha yao bila kujibakiza kwa ajili ya kuwahudumia wake kwa waumi wahitaji . Krsimas Njema alimalizia Papa.








All the contents on this site are copyrighted ©.