2013-12-25 11:43:46

Noeli ni wakati muafaka wa kukutana na Yesu Kristo!


Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema wanasherehekea Siku kuu ya Noeli, yaani kuzaliwa kwa Yesu Kristo Mkombozi wa ulimwengu. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawaambia kwamba, Noeli ni Siku kuu ambayo Yesu Kristo anakuja kati ya watu wake; huu ndio wakati muafaka wa kila mwamini kujitahidi kukutana binafsi na Yesu Kristo, Bwana na Mkombozi.







All the contents on this site are copyrighted ©.