2013-12-25 08:39:28

Ni Noeli ya Bwana!


Baba Mtakatifu Francisko kwa mara ya kwanza kama Khalifa wa Mtakatifu Petro ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye kesha la Siku kuu ya Noeli; ibada ambayo imefuatiliwa na vituo vya televisheni 65 kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Ibada ya Misa Takatifu imekamilika kwa Baba Mtakatifu Francisko kubeba Sanamu ya Mtoto Yesu na kuipeleka Pangoni, kiashilia cha Siku kuu ya Noeli.

Wakati wa Noeli mchana, Baba Mtakatifu Francisko atatoa salam na ujumbe wa Noeli kwa mji wa Roma na Ulimwengu kwa ujumla kama unavyojulikana kwa lugha ya Kilatini, Urbi et Orbi, kuanzia saa 6:00 mchana kwa saa za Ulaya.







All the contents on this site are copyrighted ©.