2013-12-25 15:14:14

Baba Mtakatifu Francisko asema, Ukristu ni hija ya maisha


Jumanne Usiku Papa Francisko aliongoza Ibada ya Mkesha wa Noel katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro majira ya saa tatu na nusu za usiku. Katika homilia yake alisisitiza kwamba waamini wa Kanisa ni watu mahujaji wanaotembea ambao wameuona mwanga wa kuwaongoza katika njia inayoelekea kwenye uzima wa milele. Kwamba, ni watu waliotembea katika giza na sasa wameouna mwanga mkubwa (Isaya 09:01 ).
Papa alieleza, kwamba, unabii huu wa Isaya, daima hutugusa sisi , na hasa wakati tunaposikiliza liturujia ya Mkesha wa Noel. Jambo hili si kama ni hisia au kwamba ni la kufikirika, la hasha, bali ni ukweli halisi , na linatugusa kwa sababu linataja ukweli wa kina juu yetu kwamba , sisi ni watu wasafiri, tunasafiri na wote waliotuzunguka pande zote, na miongoni mwetu pia kwa sababu katika safari hii, tunatembhea na yote mawili, katika uchaguzi wetu, kati mwanga na giza.

Katika Usiku huu , wakati roho wa giza anatoweshwa ulimenguni na mwanga mpya unaibuka kama maajabu ya kushangaza , wasafiri wanaouona mwanga mkuu . Mwanga ambayo unatufanya sisi kama wasafiri kutafakari juu ya siri hii: siri ya kutembea na kuona.

Papa alifafanua kwamba, Neno hili, linatufanya sisi kutafakari juu ya mwendo wa historia hii ya wokovu, safari ya muda mrefu , ambayo ni historia ya wokovu, kwa kuanzia na Ibrahimu, Baba yetu katika imani , -ambaye Bwana siku moja alimwita na kumtaka atoke katika nchi yake kuelekea katika nchi atakayo mwonyesha.

Papa alisema, tangu wakati huo, utambulisho wetu kama waumini, umekuwa ni watu wasafri walio katika hija ya maisha , watu wanaotembea kuielekea nchi ya ahadi. Na historia hii daima imekuwa ikisindikizwa na Bwana , ambaye daima ni mwaminifu katika kutimiza maagano na ahadi zake. Mungu ni mwanga, na ndani yake hakuna giza (1 Yoh 1:05 ). Hata hivyo kwa upande wa watu,kuna wakati wa yote mawili , kipindi cha mwanga na kipindi cha giza, kipindi cha uaminifu na ukafiri, utii, na uasi, wakati wa kuwa watu Hija na wakati wa kujitenga.

Na kwamba, katika historia yetu binafsi pia , kuna yote mawili wakati wa mwanga mkali na giza nene , taa na uvuli. Kama tunampenda Mungu na ndugu zetu wake kwa waume, hapo tunatembea katika mwanga, lakini kama dhamiri yetu imefungwa , na kukubali kuongozwa na kiburi , udanganyifu, ubinafsi , basi tuko katika giza, tumefunikwa na giza ndani mwetu na mazingira yanayotunzunguka yote ni giza. Kila anayemchukia ndugu yake - anaandika Mtume Yohane;yu ndani ya giza , anatembea gizani, na hajui wapi anapoelekea kwa sababu giza limepofusha macho yake. (1 Yoh 2:11).

Papa alieleza na kurejea jinsi wachungaji wa kwanza walivyopokea habari hii ya kuzaliwa kwa Yesu. Na kwamba walikuwa wa kwanza kwa sababu walikuwa na macho kuuuona mwanga uliomulikia mbingu na dunia. Pamoja nao , tumshukuru Mungu kwa kutupatia Yesu kuja kukaa kati yetu. Na pamoja nao na tuinue kutoka ndani ya mioyo yetu sifa na shukurani kwa uaminifu wake.

Papa aliendeela kutolea sala na shukurani kwa Bwana akisema, tunakutukuza, Bwana Mungu uliye juu, uliyekubali kujishusha kwa kwa ajili yetu. Wewe uliye mkuu umejifanya mwenyewe kuwa ndogo, wewe uliye tajiri na umejifanya mwenyewe kuwa maskini, wewe mwenye nguvu zote na umejifanya mwenyewe kuwa mnyonge na kuzaliwa katika mazingira magumu.

Papa alimalizia homilia yake akitoa mwaliko kwa Wakristu wote, kushirikishana furaha ya Injili , akisema, Mungu anatupenda sote , na anatupenda kiasi cha kumtoa nwanae pekee kuwa ndugu yetu, na kuwa mwanga wa kuondoa giza letu. Na kwamba Bwana anarudia tena kusema, tusiongope, (Lk 2:10). Na hivyo Papa pia alirudia kusema, Hakuna kuogopa. Baba Yetu ni mvumilivu, yeye anatupenda sisi , ametupa Yesu kutuongoza sisi katika njia inayoongoza katika nchi ya ahadi. Yesu ni mwanga wa mapambazuko. Yeye ni amani yetu. Amina.








All the contents on this site are copyrighted ©.