2013-12-24 09:31:05

Iraq inasherehekea Noeli 2013 kama Siku kuu ya Kitaifa!


Kwa mara ya kwanza katika historia ya Iraq, wananchi wote wanasherehekea Siku kuu ya Noeli kama Siku ya Mapumziko Kitaifa. Serikali imetoa uamuzi huu baada ya Patriaki Louis Sako wa Kanisa la Wakaldei kuwasilisha ombi hili rasmi kwa Serikali ya Iraq.

Hata hivyo Serikali inasema, ombi hili kwa ni kwa ajili ya Noeli ya Mwaka 2013 tu. Habari hizi zimethibitishwa na Patriaki Louis Sako mwenyewe! Anasema hizi ni alama za matumaini hata kwa siku za usoni!







All the contents on this site are copyrighted ©.