2013-12-23 11:34:34

Papa Francisko atembelea Hospitali ya watoto -Roma


Jumamosi Desemba 21 ,Baba Mtakatifu Francisko alitembelea hospitali ya watoto ya mjini Roma ya Bambino Gesu ambayo iko katika kilima cha Gianicolo , Piazza S. Onofrio 4 - Rome . Mmiliki wa Hospitali hiyo ni Vatican, na ni Hospitali kubwa ya watoto na kituo cha utafiti kwa maradhi ya watoto barani Ulaya , kinachofanyakazi kwa mshikamano na vituo vingine vya kimataifa, katika juhudi za kutibu watoto wagonjwa.

Katika ziara hii Papa alikutana na umati wa watu wasiopungua elfu nne katika uwanja wa hospitali hiyo, wakiwepo watoto wagonjwa na vijana wa kituo cha huduma na familia zao , ikiwa ni pamoja na wataalamu wa afya, wafanyakazi na watendaji wengine, wote waliofika kumtakia mema Papa kwa maadhimisho ya Siku Kuu na Noel na mwaka mpya.

Nae Papa katika hotuba yake, aliwahakikishia sala zake , watoto wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hiyo na kwingineko , matashi mema ya Noel na mwaka mpya, na aliwashukuru kwa kushirikishana nae ndoto zake , kupitia maombi yao, ambayo wameyaandika katika karatsi zilizo kusanywa katika kikapu na kisha kumpatia. Aliwatia moyo kwamba, Yesu yu pamoja nao na ndiye mwenye kujua yote kuliko mtu yeyote - Yeye anajua yaliyo katika mioyo yao, na hasa kwao watoto , Yesu ana dhamana maalum : Yeye daima yu karibu na nao.

Hospitali ya Bambino Gesu , Ilianzishwa mwaka 1869, na ina maendeleo ya kiwango cha juu katika utaalamu wa kutibu watoto, na hupokea watoto si kutoka Roma au Italia tu , lakini pia kutoka nchi jirani ya Ulaya.

Ziara ya Papa Francis inaendeleza utamaduni ulioanza mwaka 1958, wakati Papa Yohane John XXIII alipotembelea hospitali kwa mara ya kwanza. Na Papa Paul VI alitembelea hospitali Januari 1968;. Pia Papa Yohane Paul II , aliizuru hospitali hiyo Januari 1979, na Papa mstaafu Benedikto wa XVI aliendeleza utamaduni huo kwa kuzuru hospitali ya Bambino Gesù mwezi Septemba 2005.
Moja ya lengo kuu la ziara ya Baba Mtakatifu Franscisko katika Hospitali hii , Jumamosi Desemba 21, 2013 , ilikuwa ni utawala wa Hospitali, kuwasilisha juhudi mpya za kuwa na Nyumba inayoitwa “Nyumba ya Francisko”, ambapo patakuwa ni mahali pa salama, kwa ajili ya kuwapokea na hudumia wamama mama na watoto wanaotoka katika hali ngumu, waliotupwa pembezoni na jamii au kuishi katika mazingira hatarishi. Mradi huu wa Nyumba ya Francisko, unatazamia kujenga mazingira ambayo mama na watoto watapokelewa na kukubalika, kisaikolojia na kwezeshwa kupata msaada kijamii, hasa kupitia elimu, katika mtazamo wa kumfanya mama mgeni ajisikie salama na kuweza kusimama katika miguu yake mwenyewe na kuendelea na maisha kama kawaida.
Hospitali ya Bambino Gesù, inahudumiwa na jumla ya wafanyakazi 2600, wakiwa ni madaktari , watafiti, wauguzi, mafundi na wahudumu wa kawaida. Kwa mwaka huhudumia zaidi ya wagonjwa milioni 1, wagonjwa wa nje wakiwa wastani wa 27,000 hospitalini , wale wanaofanyiwa upasuaji 25,000 na huhudumia kwa wastani matatizo ya kidharura 71,000. Kuna jumla ya vitanda vyakulaza wagonjwa 607 .
Hospitali hii ya Bambino Gesu, ilianzishwa mwaka 1869 kama hospitali ya kwanza kwa watoto nchini Italia ( kwa ajili ya mpango ukarimu wa Binti Mfalme Arabella na Scipio Salviati ). Na kunako mwaka 1924, kilitolewa kama zawadi kwa Kiti kitakatifu na hivyo pia ikafahamika kama Hospitali ya Papa.
Watoto wote waliolazwa Giannicolo, waliweza kufuatilia ziara ya Papa kwa kutazama katika luninga zilizowekwa katika vyumba vyao.








All the contents on this site are copyrighted ©.