Jumuiya ya Kimataifa inawataka viongozi wa Sudan ya Kusini kuanza majadiliano ili
kurejesha amani na utulivu!
Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wa Rais Sudan ya Kusini Bwana Riek Machar wameamua
kufanya mazungumzo yasiyokuwa na masharti kama njia ya kurudisha tena amani na utulivu
Sudan ya Kusini ambayo hivi karibuni imejikuta ikitumbukia katika vita ya wenyewe
kwa wenyewe na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu!
Taarifa za kidiplomasia
zinabainisha kwamba, viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wanapingana ameamua kufuata
ushauri uliotolewa na Mawaziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa
kutoka Umoja wa Afrika. Rebecca Garang, mjane wa John Garang ameonesha nia ya kushiriki
katika mazungumzo haya.
Jumuiya ya Kimataifa inawataka viongoni wa Sudan ya
Kusini wanaopinga kuonesha utashi wa kisiasa kwa kusitisha mapigano, ili amani na
utulivu viweze kutawala tena. Machafuko ya kisiasa na kijamii nchini Sudan ya Kusini
yanatishia amani na usalama Ukanda wa Afrika Mashariki na kati!