2013-12-20 11:40:46

Onesheni ukarimu kwa kulitegemeza Kanisa!


Kardinali Thèodore Adrien Sarr, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dakar, Senegal, hivi karibuni amewataka waamini na watu wenye mapenzi mema kujisadaikisha zaidi, ili kukamilisha ujenzi wa Madhabahu ya Jimbo yaliyowekwa chini ya usimamizi wa Mtakatifu Paul de Grand Yoff.

Anasema, inasikitisha kuona kwamba, waamini wanakuwa wachoyo na kukosa ukarimu kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kanisa mahalia. Kila mwamini akijitosa kimasomaso kuchangia ujenzi wa Kanisa, mafanikio makubwa yanaweza kuonekana mara moja. Ustawi na maendeleo ya Kanisa mahalia ni dhamana inayopaswa kutekelezwa na waamini wenyewe.

Kardinali Sarr anawashukuru waamini ambao wanaendelea kuchangia kwa hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa Kanisa, ulioanza kunako Mwaka 2000, mara tu alipoteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dakar, Senegal. Madhabahu haya ni muhimu sana katika mikakati ya shughuli za kichungaji, Jimbo kuu la Dakar, Senegal. Hapa kuna Kanisa la Parokia, ujenzi wa Chuo kikuu; Chuo cha ufundi na uuguzi.

Kardinali Sarr anasema mradi huu umepanuliwa ili kuhakikisha kwamba, Jimbo kuula Dakar, Senegal linapata mahali ambapo waamini wanaweza kushiriki kwa idadi kubwa kwani Kanisa kuu la Jimbo kuu la Dakar kwa sasa ni dogo na haliwezi kukidhi mahitaji ya ongezeko kubwa ya idadi ya waamini wanaoshiriki katika Ibada mbali mbali. Gharama za ujenzi wote hadi kukamilika zinakadiriwa kuwa ni Euro millioni 4. 5







All the contents on this site are copyrighted ©.