2013-12-20 13:35:10

Bwana James Bebaako-Menshah awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 20 Desemba 2013 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana James K. Bebaako-Mensah, Balozi mpya wa Ghana mjini Vatican. Bwana Bebaako- Mensah, alizaliwa tarehe 11 Novemba 1941. Ameoa na ana watoto watano. Kuanzia maka 1965 hadi mwaka 1991 alipata fursa ya kujinoa katika nyanja mbali mbali za maisha.

Ni mwanasiasa aliyebobea katika masuala ya uongozi. Kwa miaka mingi amekuwa ni Katibu mkuu katika Wizara mbali mbali nchini Ghana. Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2013 alikuwa ni Katibu mkuu wa Rais nchini Ghana.







All the contents on this site are copyrighted ©.