Waziri mkuu Ralph Gonzales akutana na kuzungumza na Papa Francisko mjini Vatican
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 19 Desemba 2013 amekutana na kuzungumza
na Bwana Ralph Everard Gonsalves, Waziri mkuu wa wa San Vincenzo na Grenadine. Baadaye
Waziri mkuu amezungumza pia na Askofu mkuu Pietro Parolin katibu mkuu wa Vatican na
ujumbe wake.
Katika mazungumzo baina ya viongozi hawa wawili, wamegusia umuhimu
wa Jamii kusimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai na tunu msingi za maisha
ya ndoa na familia; elimu ipewe kipaumbele cha pekee sanjari na majadiliano ya kidini,
ili kudumisha haki na amani.
Viongozi hawa wameonesha nia yakutaka kudumisha
uhusiano kati ya nchi hizi mbili na kuendelea kushirikiana katika medani za Jumuiya
Kimataifa.