2013-12-19 15:29:13

Mtu mmoja anashikiliwa kwa kujiunguza kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican


Jeshi la Polisi nchini Italia linachunguza ajali ya mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 51 aliyejiunguza mwilini mwake kwenye uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican na kusaidiwa kuzima moto huo na Wasamaria wema waliokuwa karibu na eneo la tukio hili.

Mtu huyo baada ya kupewa huduma ya kwanza amelazwa kwenye Hospitali ya Mtakatifu Eugenio, iliyoko mjini Roma. Bado sababu za mtu huyu kujiunguza hazijajulikana. Pembeni mwake kulikuwa na karatasi yenye namba ya simu za binti yake. Inasemekana mtu huyu ameoa na anafanya kazi ya kutembeza bidhaa barabarani.







All the contents on this site are copyrighted ©.