2013-12-19 15:22:23

Mchakato wa maboresho ya huduma zinazotolewa na vyombo vya mawasiliano ya jamii vya Vatican


Tume ya Kipapa inayopembua kuhusu shughuli za kiuchumi na kiutawala mjini Vatican kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za zabuni, imeikabidhi Kampuni ya McKinsey kufanya upembuzi wa kina kuhusiana na vyombo mbali mbali vya mawasiliano ya Jamii vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Vatican, ili kutoa ushauri unaopania kufanya maboresho ya huduma zinazotolewa na vyombo hivi katika ulimwengu wa kisasa.

Ushauri wa Kampuni hii utaisaidia Tume ya Kipapa kufanya maboresho zaidi, ili kuviwezesha vyombo hivi kutoa viwango na ubora wa kimataifa; ushauri ambao baadaye unaweza kufanyiwa kazi na Baba Mtakatifu katika mchakato wa mabadiliko yanayokusudiwa na Kanisa kwa sasa.







All the contents on this site are copyrighted ©.