2013-12-16 09:41:41

Papa awashukuru wajumbe wa Mfuko wa Domenico Tardini kwa kusimama kidete kulinda na kutetea utu na heshima ya binadamu!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili iliyopita, tarehe 15 Desemba 2013, alikutana na kuzungumza na wajumbe wa Jumuiya ya "Domenico Tardini dil Villa Nazareth" walioshiriki katika Ibada ya Misa takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Amemshukuru kwa namna ya pekee Kardinali Achille Silvestrini, Rais wa Mfuko wa Jumuiya ya Domenico Tardini, inayojielekeza zaidi katika kulinda na kutetea utu na heshima ya binadamu.

Baba Mtakatifu amewataka wanajumuiya hawa kuhakikisha kwamba, wanatumia vyema karama na vipaji walivyokirimiwa na Mwenyezi Mungu kwa mafao ya wengi ndani ya Jamii. Hiki ni kielelezo cha mshikamano wa dhati ndani ya Kanisa na kwa ajili ya Kanisa. Amewasihi kuendelea kumsindikiza katika sala na sadaka zao, ili aweze kutekeleza kwa umakini mkubwa utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.







All the contents on this site are copyrighted ©.