2013-12-16 10:55:50

Dr. Francesco Kyung-surk Kim awasilisha hati zake za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 16 Desemba 2013 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Dr. Francesco Kyung-surk Kim, Balozi wa Korea ya Kusini mjini Vatican. Bwana Kim alizaliwa tarehe 8 Juni 1948, ameoa na ana watoto wawili. Ni mtaalam wa lugha, sayansi jamii na diplomasia.

Tangu mwaka 1972 amekuwa akijiendeleza katika fani mbali mbali za maisha hadi kufikia mwaka 2012 akajipatia Shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki, Sacro Cuore, cha Milano kunako mwaka 2012.

Ni mwandiplomasia aliyebobea kwani kazi hii aliianza kunako mwaka 1984 akashika nyadhifa mbali mbali katika Wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Kwa miaka mingi amefanya kazi mjini Roma. Kati ya Mwaka 2004 hadi mwaka 2005 alikuwa ni Balozi wa Korea ya Kusini nchini Italia. Mwaka 2005 hadi mwaka 2008 alikuwa ni Balozi wa Korea ya Kusini nchini Quito. Tangu mwaka 2012 hadi mwaka 2013 alijihusisha na masuala ya utafiti kwenye Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sacro Cuore cha Milano hadi kuteuliwa kwake kuwa ni Balozi wa Korea ya Kusini mjini Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.