2013-12-14 16:01:08

Wakati ujao uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu


Imani ni fadhila ya Kimungu ambayo kwayo tunamsadiki Mungu na kila kitu alichokisema na alichotufunulia, na ambacho Kanisa Takatifu latutaka tukisadiki, kwa sababu Yeye ndiye Ukweli wenyewe. Kwa imani mwanadamu hujitoa nafsi yake yote kwa Mungu.

Ni kwa sababu hiyo mwamini hutafuta kujua na kufanya mapenzi ya Mungu. Mwenye haki ataishi kwa imani na imani. Na imani hai hutenda kazi kwa upendo.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema, tumaini la Mkristo ni kwamba: wakati ujao uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu.







All the contents on this site are copyrighted ©.